Wednesday, 29 April 2015

MZIMU WA AJALI LINI UTAKOMA ??? ULIISIKIA HIIII? SOMA CHANZO CHAKE!!



Mzimu wa ajali za barabarani umeendelea kuliandama taifa la Tanzania kadiri siku zinavyozidi kwenda, Tatizo hili la ajali za barabarani limekuwa likihusishwa na mambo mengi yakiwemo ya mwendokasi, uzembe wa madereva, ukaidi, dharau, na ushirikina .

Juzi huko mkoani Morogoro watu zaidi ya 50 wamenusurika kifo na wengine 15 wamejeruhiwa vibaya baada ya kutokea kwa ajali iliyoyahusisha mabasi ya abiria ya mikoani ya kampuni za ABOOD BUS T 830AWY  linalofanya safari zake kati ya Morogoro na Dar es salaam na basi la TAK-BIR linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Dar es salaam na Geita. Ajli hiyo ilitokea katika maeneo ya kijiji cha Lubungo mikese mokoani Morogoro ,

Majeruhi na walionusurika katika ajali hiyo walielezea kuwa chanzo cha ajli hiyo ni mwendokasi wa basi la TAK-BIR ambao ulimfanya dereva ashindwe kulimudu basi lake na kupelekea kuligonga basi la ABOOD kwa nyuma na kusababisha maafa hayo. walizidi kusema kuwa na baada ya ajali hiyo, dereva wa basi la TAK-BIR alikimbia kusikojulikana.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paulo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwaomba madereva wa magari hasa mabasi ya mikoani kuwa makini na kutoendesha magari ya kwa mwendo kasi kiasi cha kushindwa kuyamudupindi itokeapo dharula kama hiyo!

BREAKING NEWS!! SUMATRA YAIONYA TABOA , ATAKAEGOMA TUNAMFUNGIA LESENI YA USAFIRISHAJI ABIRIA TANZANIA!!!!!



MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), wamesema hawajapata taarifa rasmi juu ya mgomo wa wamiliki wa mabasi ya mikoani.
Akizungumza na MPEKUZI  kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari wa Sumatra, Daud Mziray, alisema hakuna taarifa yoyote iliyowafikia ofisini kwao ya wanachama wa Taboa kugoma.
“Mimi niko mkutanoni Morogoro, mkutano wenyewe unahusiana na mambo ya ajali, hatujapata taarifa rasmi ya wanachama wa taboa kugoma,”alisema Mziray.
MPEKUZI ilimtafuta Katibu wa Taboa, Enea Mrutu, ili kuzungumzia suala hilo ambapo alisema kuwa tayari wameshapeleka barua yao Sumatara leo (jana) saa moja asubuhi na tamko lao ni lilelile waliloadhimia katika mkutano wao.
“Sumatra tumekwisha wapelekea barua toka saa moja asubuhi kama wanasema hawana tarifa wanadanganya kwasababu hata jana katika kikao chetu mwakilishi wao alikuwepo.
“Ingawaje kuna taarifa nimeipata kuwa Serikali inataka ifanye mazungumzo na sisi, tutakaa nao kama wataridhia kuacha nauli kama ilivyokuwa hatuna tatizo lakini wasipofikia muafaka na kutoa majibu ya kueleweka msimamo wetu utakuwa ni uleule,”alisema Mrutu. 
Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani juzi katika mkutano wao walijadiliana juu ya kushuka kwa nauli na kuafikiana kutoshusha jambo ambalo limetafsiriwa kuwa ni kuitunishia misuli mamlaka hiyo.
Walisema endapo Sumatra hawatatoa  majibu mapema kuanzia  Aprili 29 mwaka huu  (leo) hawatokata tiketi kwa wasafiri na badala yake wataendelea na mgomo huo kwa  siku saba. 
Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu, alisema SUMATRA ilikurupuka  kushusha nauli bila kufanya mchanganuo na kuda.
Wamiliki hao waliafikiana kuwa yeyote atakayetoa gari lake kufanya biashara kabla hawajapata muafaka kutoka SUMATRA watamchukulia hatua za kisheria.
Aidha waliitaka serikali kurudisha viwango vya nauli za mabasi ya mikoani kwenye hali yake ya kawaida iliyokuwepo miezi michache iliyopita kwa sababu bei ya mafuta imerudi juu, baada ya kushuka kwa kisingizio cha bei ya mafuta kushuka.
Mpekuzi blog

Friday, 24 April 2015

BASI LA SUPER FEO KUUNGUA MOTO, HUU NDIYO UKWELI NA CHANZO CHAKE!!!!!!!!!!!!!!11


Hiki ndicho kilichosemwa na meneja wa kampuni ya super feo bw.Sengo juu ya basi la kampuni yake kudaiwa kuungua moto na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.

Kwanza Kampuni ya Super Feo Express imesikitishwa sana na taarifa hizi za upotoshaji. Tunajua hizi ni mbinu za watu wanaotaka kuchafua jina na biashara yetu. Ukweli ni kwamba basi halikuteketea kwa moto kama ilivyoandikwa na gazeti la Majira. Kulitokea hitilafu ya kuvuja kwa mafuta yaliyodondokea kwenye bomba la joto kali la kutolea moshi na hivyo wakati mafuta yanaungua ukafuka moshi uliosababisha taharuki kwa abiria. Dereva wetu alisimamisha gari na abiria wote walishuka salama. Basi halikuteketea wala kuungua moto kama ilivyoandika. Na hata baada ya abiria kushuka basi letu lingeweza kuendelea na safari lakini kwa sababu ya hali ya taharuki na hofu na pia tukizingatia kampuni yetu ina mabasi mengi kwenye vituo mbalimbali tuliamua kuchukua basi jingine pale Iringa na abiria wakaendelea na safari yao kama kawaida. Kwa hiyo nachukua nafasi hii kuwatoa hofu wananchi na wateja wetu kwamba taarifa hizi za kuteketea kwa basi la Super Feo sio kweli na wazipuuze. Daima kampuni yetu inatumia mabasi mazuri, bora na salama kwa abiria. Mabasi yetu yanafanyiwa matengenezo ya uhakika na kufungwa vipuri vya uhakika kila inapohotajika. Zaidi ya hapo Super Feo kila siku ina hakikisha wananchi wanapata kilicho bora. Na kwa sasa timu ya wataalamu inakamilisha mambo mengine mazuri kwa ajili ya kuboresha huduma zetu.

Thursday, 19 February 2015

FANYA HAYA 6 KUZUIA WATU WASIINGILIE MAPENZI YENU


Sio mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano yako wewe na mpenzi wako. Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi.  Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.


1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine:  Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.

2. Upekee wa mambo:  Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.

3. Mwenye maamuzi ni wewe: Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua. 

4. Kuwa na subira: Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka  unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza  kuzitumia kupata suluhu ya tatizo. 

5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu: Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa  nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine. 

6. Kuweni peke yenu: 
 Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni  kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi.  Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao  kumi‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.

7. Nenda ‘darasani’ :  Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu. Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu.

Watatu wauawa, 6 wajeruhiwa mapigano wakulima, wafugaji.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo.
Watu watatu wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika mapigano yaliyozuka kati ya wakulima na wafugaji katika Bonde la Kilimo cha Mpunga la Matembele, lililoko kati ya vijiji vya Mabwegere na Mbigili, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
 
Waliofariki; wawili wanatoka upande wa wakulima, ambao ni wakazi wa Kijiji cha Mbigili na mmoja ni mfugaji kutoka jamii ya Kimasai anayeishi katika Kijiji cha Mabwegere.
 
Kati ya waliojeruhiwa; wawili hali zao zinadaiwa kuwa ni mbaya na hivyo, kulazimika kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro kwa matibabu zaidi.
 
 Mapigano hayo yalizuka juzi zikiwa zimepita wiki mbili baada ya nyumba 46 zilizokuwa zikimilikiwa na baadhi ya wafugaji wa Kijiji cha Mabwegere na wakulima kuchomwa moto na kundi linalodaiwa ni la wakulima, huku wafugaji wa jamii ya Kimasai wakikimbia kuokoa maisha yao.
 
 Akizungumza na waandishi wa habari baada kuwatembelea majeruhi waliopo katika Hospitali ya Misheni ya Mtakatifu Joseph, iliyopo katika mji mdogo wa Dumila, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo, alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo pamoja na majeruhi.
 
Aliwataja waliofariki kuwa ni Joseph Peter (26) na Rajab Nasoro (55) wote wakulima kutoka Kijiji cha Mbigili na mfugaji wa jamii ya Kimasai, Kaduhu Kashu, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mabwegele. Wote walifariki baada kuchomwa vitu vyenye ncha kali katika mapigano hayo.
 
 Waliojeruhiwa ni Binzi Dotto (42) Shigele John, Juma Someke, Mohamed Athuman, Mbwana Athuman na mfugaji, ambaye jina lake halijatambulika baada ya kukimbizwa na ndugu zake katika hospitali isiyofahamika.
 
Alisema tukio hilo lilitokea juzi, majira ya kati ya saa 9 na saa 10 jioni, baada ya wakulima  wanaokadiriwa kufikia 15 kutoka katika Kijiji cha Mbigili, kwenda katika Bonde la Matembele wakiwa na matrekta kwa ajili ya kuanza kutayarisha mashamba ya kilimo cha mpunga. Tarimo alisema siku mbili kabla ya tukio hilo, aliitisha kikao cha maridhiano baina ya pande mbili hizo kwa ajili ya kupata suluhisho la mgogoro wa bonde hilo, lakini upande wa viongozi wa kijiji cha wafugaji cha Mabwegere haukufika katika mkutano huo.
 
 Aliitupia lawama Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushindwa kupeleka wasuluhishi wa mgogoro huo wa ardhi katika bonde hilo kama walivyoahidi.
 
 Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo, Milenia Shayo, alithibitisha kupokea miili ya watu wawili na mmoja kufariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo, alisema kupitia Afisa Habari wake, Nabwike Mwakatika, kuwa atatoa taarifa baada ya kutoka kwenye eneo la tukio.
CHANZO: NIPASHE

Prisons, Mbeya City waungana kuiua Yanga



Mbeya/Dar. Ni urafiki wenye shaka. Hivyo, ndivyo unavyoweza kuzungumzia hatua ya mashabiki wa Prisons na Mbeya City kuungana ili kuimaliza Yanga.


Katika kikao cha pamoja, mashabiki hao wa klabu hizo kubwa mbili za Mbeya walikubaliana kuunganisha nguvu, kuzishangalia timu zao kwa pamoja dhidi ya Yanga.


Makubaliano hayo yamefikiwa wakati Jiji la Mbeya likianza kindumbwendumbwe cha timu zake kuikabili Yanga ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Sokoine.


Kikao hicho kilichofanyika viwanja vya City Pub, mashabiki hao walikubaliana kuwa kuanzia leo watakuwa kitu kimoja ili kuishangilia moja ya timu hizo itakapocheza na timu ngeni jijini humo.


Hata hivyo, wamesisitiza kwamba timu hizo zikikutana kwenye mechi za ligi au kirafiki, mashabiki wao wataendeleza utani wa jadi kwa kila kundi kuishangilia timu yao.


Msemaji wa Mbeya City, Dismas Ten alisema mashabiki hao walikutana na kuanzisha sura mpya ya kuzishangilia timu zao na kwamba kwa kuanzia itakuwa mechi ya leo ya Prisons dhidi ya Yanga.


Shabiki wa Prisons, Tawi la Iyunga, Aden Kinyuke alisema hatua ya kuungana kwa mashabiki hao ni kuutakia mema mkoa wao ili uweze kubaki na timu mbili Ligi Kuu. Kuhusu mechi hiyo, Kinyuke alisema Prisons imejipanga kwa hali na mali kuitandika Yanga.

Tayari, Yanga imetangaza azma ya kunyakua pointi sita mkoani Mbeya kutoka kwa Prisons leo na Mbeya City, Jumapili.

Kocha Hans Pluijm alisema juzi kwamba wapo Mbeya kupata pointi na siyo kutalii na kwamba hayo ndiyo malengo yao.

Yanga, Azam zasaka pointi ugenini

Ukiacha ushabiki huo wa Mbeya, Yanga na Azam baada ya mechi zao za kimataifa, mwishoni mwa wiki zinataka kufanya vizuri kwenye ligi ambako zinakimbizana. Leo, zitakuwa ugenini kwenye michezo yao dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani ambako Azam itacheza na Ruvu Shooting.

Azam iliifunga mabao 2-0 El- Merreikh ya Sudan kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga kupata ushindi kama huo, dhidi ya BDF XI ya Botswana kwenye Kombe la Shirikisho.
zaidi>>mwananchi

Tuesday, 17 February 2015

Kikwete takes over EA Summit chair on Thursday/Tommorrow


PRESIDENT Jakaya Kikwete is expected to take over the chairmanship of the East African Heads of State Summit during the ordinary meeting of the five regional presidents in the Kenyan capital Nairobi on Thursday.

Mr Kikwete, who is also preparing to retire as the fourth head of state of Tanzania next November, is taking over the EA Authority chairmanship relay stick from President Uhuru Kenyatta of Kenya during the 16th Ordinary Summit of the East African Community (EAC) Heads of State.

An official statement from the Head of the Department of Corporate Communications and Public Affairs at the EAC Secretariat in Arusha, Mr Owora Richard Othieno, revealed that the one-day meeting will be held on Friday at the Kenyatta International Conference Centre (KICC) in the city.